Monday, October 27, 2008

MUSA BANZI

mmoja wa waandishi na wazalishaji wa filamu za bongo MUSA BANZI akitafakari jambo kwa umakini mkubwa, filamu yake iliyoko sokoni kwa sasa inakwenda kwa jina la VERONICA itafute uone nyota wapya wanavyocheza na camera halafu tuoneeee,,,,,,,,,,

Wednesday, October 22, 2008

PICHA NZURI SHURTI KWA POZI ATI!


Ni mpiga picha mahiri wa filamu za kibongo RASHID MRUTU ambaye anashikilia tuzo ya mpiga picha bora wa mwaka 2008 hapa akiwa kazini akipiga piccha za kipindi cha bongo movies kinachoruka CHANEL TEN kila alhamisi saa tatu usiku. nyuma yake ni mwigizaji wa filamu za kibongo.

Tuesday, October 21, 2008

HII NI TRELA TU, SKILIZIA PICHA KAMILI,,,,,,


Kama ni ngoma imepata wachezaji, ama miti kwa wajenzi, na kama ilivyo upele kwa mkunaji, wakati mwingine mwafaka wa kupata habari, matukio na kila lihusulo filamu za kibongo, huu ndo uga maalumu kwa ajili yetu wadau wa filamu, haya jamvi ndo hilooo kazi kwenu.