Monday, December 22, 2008

AILEEN

star wa filamu wa kifilipino ambaye ameingarisha filamu ya from china with love akitumia jina la aileen, fanya mpango uipige jicho halafu rejea hapa umwage maoni.

FROM CHINA WITH LOVE

tayari mzigo uko sokoni, na hivi ndivyo ionekanavyo kwa nje, walioitupia jicho wanasema ni viwango tu humo ndani.

Wednesday, December 10, 2008

AMA KWELI BONGO TAMBARARE!


siku hizi warembo kibao wanaingia katika tasnia ya filamu kama ilivyo mamtoni, kfupi bongo ni kama new york, au niseme bongo kama hollywood, tehe, tehe, tehe. mtoto wa kike(pichani) si mwingine zaidi ya NARGIS MOHAMED toka jukwaa la urembo mpaka kwenye kamera za filamu za kibongo. ama kweli bongo tambarare

ETI NI KWELI IRENE NDIYE MALKIA

baada ya mtoto wa kike kujichanganya katika anga la filamu za bongo, yasemekana yeye ndiye malkia wa ukweli wa movie za kibongo, na kwa sasa hata wakongwe wanaumwa vichwa juu yake, ila ati tatizo lake ni,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ni saidieni wadau ni kweli au maneno ya town tu.


Friday, December 5, 2008

HONGERA JOYCE


mkurugenzi wa local movies entertainment JOYCE KIRIA ambaye pia ni mtangazaji wa clouds fm leo anaanza safari ya kuelekea ndoa kwa kufanyiwa sherehe ya kitchen party pale maeneo ya mikocheni ROSTERS PUB. hongera shangazi joy. kwa picha zaidi za matukio ya shughuli hiyo stay tuned,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Monday, October 27, 2008

MUSA BANZI

mmoja wa waandishi na wazalishaji wa filamu za bongo MUSA BANZI akitafakari jambo kwa umakini mkubwa, filamu yake iliyoko sokoni kwa sasa inakwenda kwa jina la VERONICA itafute uone nyota wapya wanavyocheza na camera halafu tuoneeee,,,,,,,,,,

Wednesday, October 22, 2008

PICHA NZURI SHURTI KWA POZI ATI!


Ni mpiga picha mahiri wa filamu za kibongo RASHID MRUTU ambaye anashikilia tuzo ya mpiga picha bora wa mwaka 2008 hapa akiwa kazini akipiga piccha za kipindi cha bongo movies kinachoruka CHANEL TEN kila alhamisi saa tatu usiku. nyuma yake ni mwigizaji wa filamu za kibongo.